Bernard James
KIKOSI cha Polisi cha Kupambana na
Dawa za Kulevya mkoani Lindi, kimekamata kilo 210 za Heroine, kiasi ambacho ni
kikubwa kukamatwa tangu kuanzishwa kikosi hicho mwaka1990.Kukamatwa kwa dawa
hizo juzi, kulikuja baada ya polisi kuvamia nyumba ya mkazi wa Mchinga II na
kukuta kiasi hicho.
Mkuu wa Kikosi cha Polisi cha Kuzuia
Dawa za Kulevya Nchini, Godfrey Nzowa, alithibitishia habari hizo juzi kwa njia
ya simu.Alisema katika nyumba hizo, polisi walikutana watu watatu wakijiandaa
kusafirisha dawa hizo kwenda jijini Dar es Salaam.
“Baada ya kupoka taarifa kutoka kwa
msiri wetu nilituma vijana wa kikosi chetu cha ambao kwa kushirikiana vyema na
wenzao wa Lindi, walifanikisha kuwakamata watuhumiwa,” alisema Nzowa.Alisema
kiasi cha dawa zilizokamatwa ni kikubwa kuwahi kutokea tangu kitengo chake
kilipoanzishwa miongo miwili iliyopita.
Nzowa alisema wafanyabiashara wa
dawa hizo ambao awali walipendelea zaidi kupitia Bandari za Tanga na Bagamoyo
sasa wameamua kuingilia Bandari za Lindi na Mtwara.
Alisema hali hiyo inatokana na kuimarishwa kwa shughuli za ukaguzi katika Bandari ya Tanga na maeneo ya Bagamoyo.
Alisema hali hiyo inatokana na kuimarishwa kwa shughuli za ukaguzi katika Bandari ya Tanga na maeneo ya Bagamoyo.
Kukamatwa kwa shehena hiyo, kumekuja
miezi kadhaa baada ya Umoja wa Mataifa kuonya kuwa Afrika Masharikil imekuwa
ikipokea kiasi kikubwa cha Heroine kutoka Afghanistan na Iran na kwamba hiyo
inatokana na ukanda kuwa njia rahisi ya kusafirishia dawa hizo kwenda Ulaya,
Amerika Kaskazini na sehemu nyingine za dunia.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wafanyabiashara wa
dawa za kulevya wanatumia vizuri uwezo mdogo wa kiulinzi katika bandari and
viwanja vya ndege kushamirisha biashara yao.
agnesshija2005@yahoo.com
agnesshija2005@yahoo.com